THE MARATHON CHAMPION

GWIJI WA MBIO ZA NYIKA

×

Komen alikuwa akielekea shuleni Jumatatu alipomuona bibi huyo.Alikuwa anaendesha gari aina ya Passat.Kitu kilichomshangaza Komen ni jinsi huyo bibi alivyoliendesha gari hilo.

Aliliendesha gari hilo polepole sana na alionekana kama mwenye alikuwa anajifunza kuliendesha gari, yaani mwanafunzi mkongwe sana wa kuendesha gari.

Huyo bibi alionekana kama mwenye ana miaka arubaini na tano.Komen alimuonyesha alama ya kobe.Huyo bibi alipoiona hiyo alama akamuonyesha alama ya kuchinja.

Komen alipofika shuleni, alikuwa amesahau yote kuhusiana na yule bibi. Ilikuwa ni kwa sababu alikuwa amechelewa na alijua angeadhibiwa na mwalimu wa zamu.

Nyumbani kwa kina Komen kulikuwa mbali sana na shule. Lakini hili halikuwashughusha walimu.

La muhimu kwao ni kila mwanafunzi afike shuleni kwa wakati unaofaa, yaani saa moja u nusu asubuhi.

Baada ya kuadhibiwa na mwalimu wa zamu, Komen aliingia darasa la saba.Alimpata mwalimu wa Isabati akiendeleza somo la hesabu.

Mwalimu Muniafu, mwalimu wa hesabu, alimuadhibu kwa kuchelewa kuingia darasani.

Kwa sababu Komen alikuwa mwanafunzi mchangamfu,hakuruhusu kuadhibiwa kuharibu siku yake.Alikuwa amesahau haya yote na hata bibi wa Passat wakati wa mapumziko.

Siku ya Jumanne, Komen alichelewa tena kuenda shuleni na akamwona huyo bibi wa Passat kwa mara ya pili.Komen alimuonyesha tena hiyo alama ya kobe.Bibi huyo akamuonyesha ilea lama ya kumnyonga.

Alitabasamu huku akikimbia kuelekea shule.Alijua amekutana na mtu anayedhaniana naye.Hii ilifanyika mpaka Jumatano.

Jumamosi ilikuwa siku ya shule lakini kwa wanafunzi wa darasa la saba na nane.

Ilikuwa siku ya mapumziko. Hivyo basi wanafunzi waliruhusiwa kuingia shuleni saa mbili asubuhi badala ya saa moja u nusu.Hiyo Jumamosi, Komen hakujua kuwa itabadili maisha yake milele.

Komen alitoka nyumbani saa kumi na mbili u nusu.Kama ilivyo desturi yake, alikimbia polepole akielekea shuleni.Alipofika pahali pake pa kawaida alimuona huyo bibi.

Huyo bibi alikuwa kwa gari lake la kawaida na alikuwa anasafiri kuelekea upande alikokuwa anatoka Komen.Kama ilivyokuwa mazoea ya Komen, alimuonyesha alama ya kobe.

Lakini kwa wakati huu, bibi huyu hakumuonyesha alama ya kuchinja badala yake alilisimamisha gari lake kwa ghafla.

Aliachilia gari likarudi nyuma kidogo na liliposimama, alitoka akiwa na ufunguo mkononi.Hii yote ilifanyika kwa muda uliokuwa mfupi sana.

Huyo bibi alipovuka barabara kuelekea upande alipokuwa Komen, ndipo Komen akatambua anmwandama.Alianza kukimbia na huyo bibi naye akaanza kukimbia akimfuata.

Komen alihisi uoga. Alishangaa jinsi bibi huyu alikuwa na hatua ndefu.

Ingawa huyu bibi hakuwa mrefu, alikuwa na miguu mirefu. Ngozi yake ilikuwa ya maji ya kunde na nywele zake zilikuwa ndefu.

Ilikuwa rahisi kubaini kuwa alikuwa na siha njema.Umri wake ulikuwa miaka arubaini na tano.

Hii ilikuwa mbio ngumu sana ambayo Komen aliwahi kushiriki.Komen alikimbia kwa kasi sana lakini huyo bibi alimfuata kwa mwendo uo huo.

Hakuna mtu alionekana mbele yake.Mbele kidogo kulikuwa na kijilima.Komen alidhania kwamba bibi huyu atakufa moyo mara tu watakapoanza kupanda kile kijilima.

Hii ingetokana na umri mkubwa wa huyo bibi na pia alikuwa mwanamke.

Komen alipofika mlimani aligeuka kidogo ili aone kama huyo bibi amekufa moyo.Alistajabu alipogundua kuwa amemkaribia badala ya kubaki nyuma.

Kwa wakati huu Komen alikuwa anapumua kwa shida.Alitokwa na jasho huku akihema sana na pumzi yake ikitoka kwa mshindo.Haya yalibaini uoga na kukimbia kwa mwendo wa kasi sana.

Aling’ang’ania kufika pahali ambapo pana watu kwa sababu hakujua lengo la mwanamke yule.

Alivyojikakamua ndivyo yule mwanamke alivyojikakamua.

Komen alidhani kuwa kungekuwa na watu karibu na mto kwani ilikuwa desturi kuwapata wanawake ambao walifika hapo kuchota maji.Lakini hakuwa mtu karibu na mto.

Mto ulikuwa kati ya shule na kwao nyumbani.Aligundua kuwa atakimbia mpaka shuleni.

Hii ni kwa sababu alijua hakutakuwa na mtu mpaka huko shuleni. Aliijua hiyo barabara vyema.

Alihisi kama mtu aliyekimbia kwa miaka mingi bila kupumzika.Mdomo wake ulikauka sana.Alikuwa Karibu kuzirai.kifua chake kilikuwa ni kama kinaungua.

Hapo ndipo aliinua kichwa chake na kuona mlango wa shule yao kwa umbali.

Alipokuwa akijaribu kukimbia kwa kasi zaidi ndipo aufikie mlango wa shule yake, huyo bibi aliongeza mwendo na kumpita Komen.Hakujaribu hata kumgusa Komen.

Komen alipoona kwamba huyo bibi ameenda mbele yake, aliinama ili apate kupoa kidogo.Huyo bibi alikimbia hadi kwa lango la shule, halafu akapinduka na kuanza kukimbia akirudi alikokuwa Komen.

“Hujambo Gwiji?” Huyo bibi alimsalimu Komen.

Alitamka neno Gwiji kama jina lake Komen.

“Jina langu siyo Gwiji.Ninaitwa Komen,” Komen alisema huku akipumua kwa shida.

Hakuhisi uoga wowote kwa sababu sasa alikuwa karibu sana na shule yake.

“Tumekimbia mwendo wa kilomita kumi kwa muda wa dakika thelatini.Huo ni mwendo sawa na mwanaridha mkuu wa Riadha za Marathon.Kwa hivyo mimi nakuita wewe Gwiji," huyo bibi akamwambia.

Komen alitaka kujua jambo.

“Je wewe ni mmoja wao?” Alimuuliza huku akimwangalia kwa karibu.

"Nilikuwa mmoja wao miaka kumi na miwili ilyopita.Sasa nimestaafu lakini bado huwa nakimbia kwa mashindano ya vijijini.Kutakuwa na Karbarnet Nusu Marathon Jumamosi ijayo.

Zawadi ya mshindi itakuwa shilingi elfu mia mbili.Je utajaribu?”

“Ahsante lakini sitaweza.Nitakuwa shuleni.”

“Ni sawa.Kimbia uende shuleni usije ukachelewa.” Halafu huyo bibi alitimua mbio akaenda zake.

Komen alimwangalia huyo bibi akikimbia akielekea kulikokuwa gari lake.Hakukimbia kwa kasi sana lakini alikimbia kwa mwendo bila kupunguza.

Komen alitambua siri ya kwanza ya magwiji: enda kwa mwendo uo huo au ongeza mwendo lakini usipunguze mwendo.

Komen alishangaa wakati alipoingia shuleni alipotambua kwamba ni saa moja na dakika kumi tu. Wanafunzi wengine walimtazama sana.

Hapo akatambua ya kwamba alikuwa anahema sana na ametoa jasho nene.Jumatatu iliyofuata baada ya mbio na bibi wa gari la Passat, Komen alifika shuleni saa moja na nusu.

Alikuwa anatoa jasho lakini la muhimu ni kwamba hakuadhibiwa kwa sababu ya kuchelewa.Alikuwa ametumia dakika arubaini pekee.

Siku ya Jumanne, Komen alifika shuleni saa moja na dakika ishirini na tano.Baadaye, akawa anafika shuleni saa moja na nusu au saa moja na dakika ishirini na tano.Hakuadhibiwa tena kwa kuchelewa.

HAYA YOTE YALIFANYIKA wakati Komen alikuwa bado katika shule ya msingi.Alifanya mtihani wa darasa la nane mwaka uliofuata na akafanikiwa kujiunga na shule ya upili ya Iten.

Ilikuwa huko ndiko alikotambua kwamba kuwa mkimbiaji mashuhuri ni kitu cha dhamana sana.

Jambo la kwanza alilolitambua alipofika Iten ni kwamba wanafunzi wote walikuwa wanaruhusiwa kwenda kukimbia kila siku ya shule.

Mkufunzi wa mbio alikuwa mwalimu mkuu wa hiyo shule.Mwalimu mkuu wa shule hiyo alikuwa ni mwanamume mrefu wa kimo aliyeitwa Bwana Koech Arap Samoei.

Bwana Arap Samoei alifuatilia sana mambo ya riadha.Alikuwa na ratiba maalum ya riadha kwa afisi yake ambayo ilifuatwa na kila mwanafunzi wa hiyo shule.

Walifuata njia iliyowapitisha kwenye vijilima soko ya Tengecha.Baadaye waliingia msitu ulio na baridi nyingi na kurejea hadi shuleni.

Kuongezea; kwa msitu na vile vilima kulikuwa na vijito viwili ambavyo havikuwa na daraja.Iliwabidi wanafunzi kuvuka hivi vijito kwa kuingia majini.Saa kumi na moja asubuhi maji haya huwa baridi mno.

Hivyo vijitHizo mbio zilikuwa viliharibu vyatu vya wanafunzi.Hizo mbio zilikuwa umbali wa kilomita ishirini na mbili.

Wengi wa wanafunzi hawakuwa na viatu vya michezo lakini hiyo haikuwa kijisababu.Kila mwanafunzi lazima akimbie Jumatatu asubuhi.

Siku ya Jumanne, Mchakamchaka yaani mbio ilikuwa tu kwa wale wanafunzi waliokuwa wanapenda riadha.Nazo hizo mbio zilikuwa saa kumi na moja ya asubuhi.

Walinzi wa lango la shule waliwaruhusu kutoka nje ya lango mara tu ilipofika saa hiyo.Siku ya Jumatano, kukimbia kulikuwa ni lazima.Lakini wakati huu zilifanyika saa kumi baada ya madarasa.

Mbio ya Jumatatu zilikuwa asubuhi sana wakati kulikuwa na baridi nyingi.Lakini za jumatano zilikuwa wakati kuna jua kali sana.

Jumapili hakuna mwanafunzi aliruhusiwa kwenda nje ya shule.

Kosa kubwa ambalo mwanafunzi angefanya shuleni ilikuwa ni kukosa kushiriki mbioni. Mwanafunzi aliyefanya makosa haya alitumwa nyumbani ili amlete mzazi kasha baadaye alipewa kiziki ang’oe.

Kulikuwa na viziki vingi shuleni.Shule ya Iten ilikuwa na viwanja kumi.Hivi viwanja vyote vilikuwa na laini za mbio.

Shule ilikuwa na hekari mia tatu ya shamba.Mwalimu mkuu wa shule alikuwa na mpango wa kuvitengeza viwanja kumi na vitano kwa ajili ya michezo shuleni.

KOMEN ALIZOEA KUFUATA UTARATIBU wa shule bila shida yoyote.Alikuwa anapenda mbio.Baada ya kuwa kwa shule kwa muda mfupi, alijizoesha kwenda mbio kila siku.

Alikuwa anajipanga kushindana na Tenai. Tenai ndiye alikuwa gwiji wa mbio shuleni humo.Kila mtu alijua kwamba hakuna yeyote ambaye angeweza kukimbia kama Tenai shuleni.

Tenai alikuwa kijana mrefu an mwembamba sana.Alikuwa na umri wa miaka kumi na nane. Alikuwa na ngozi nyeusi ti ti ti.Tenai hakuwa mcheshi. Alikuwa anapenda tu kuongea juu ya kitu kimoja yaani riadha.

Wakati komen alikuwa katika kidato cha kwanza, Tenai alikuwa katika kidato cha tatu.Tenai alikuwa akikimbia kila siku. Kwa muda wa miaka miwili kabla ya Komen kujiunga na hiyo shule, hakua aliyemshinda Tenai.

Tenai alikuwa akimaliza mwendo huo kwa dakika hamsini na sita ilhali wengine wote walimaliza baada ya saa moja.

Komen alianza kujifunza kukimbia kama Tenai siku ya kwanza alipoenda kukimbia. Alitambua kwamba Tenai hakuanzia kwa mwendo wa kasi.

Lakini aliongeza mwendo vile alivyokaribia kumalizia. Baadaye alikimbia kwa kasi sana alipokuwa amebakisha kilomita moja.

Katika muhula wa pili wa huo mwaka, Mashindano ya Nusu Marathon ya Shule ya upili ya Iten yalifanyika.Washindani wakuu walikuwa Tenai ambaye alikuwa gwiji na Kiplimo.

Hakuna aliyefikiri Komen angeweza kushinda.Mbio zilipangwa kuanza saa moja u nusu asubuhi.Lakini kabla ya mbio, mwalimu mkuu alihutubu.

“Habari ya asubuhi magwiji. Hili ni muhimu sana. Kumbuka kwamba hili linaweza kuwa njia yako ya kujikimu maishani.Na wengi wamenawiri sana katika ukimbiaji.

Wamepata pesa kutokana na mbio. Sisi kama walimu tumefanya kazi kwa miaka zaidi ya ishirini lakini hatujawahi kupata hata million moja.Lakini waangalie magwiji wetu.Kwa mfano Kipchoge.Mwangalie Paul Tergat na umwangalie Tecla Lorupe.

Hawa wote wana mamillioni kutokana ukimbiaji.Nisikilize vizuri.Mimi sikufikiria kuwa ningekuwa tajiri kupitia kwa ukimbiaji.Baba yangu alinisisitizia kutia bidii masomoni tu.

Kwa hivyo nilifanya kazi kwa bidii na bado nafanya kazi kwa bidii. Lakini ningerudishwa kwa siku zangu za shule leo hii ningekuwa mwana riadha.

Ndio nataka kubadili maisha yenu kupitia riadha. Kimbieni kabisa vijana wangu.

Mshindi wa leo atalipiwa karo yake yote ya mwaka ujao.Tena atapewa shilingi elfu kumi na mbili kama pesa za matumizi ya mwaka ujao.

Natangaza sasa kufunguliwa rasmi Mbio za Magwiji wa Iten.Ahsanteni.”

Wanafunzi hao hawakuwa na hoja na karo kulipwa.Hao walifikiria tu juu ya elfu kumi na mbili za matumizi.

Ilikuwa pesa nyingi kwa vijana ambao walikuwa wamezoeshwa shilingi mia tano kama pesa za matumizi kwa muhula mzima. Komen alianza hizo mbio pole pole lakini alihakikisha kwamba anakaa karibu na Tenai na Kiplimo.

Hakujali hao vijana wengine. Kwake aliwaona tu kama wale wawekaji mwendo.Wote wangechoka sana baada ya nusu kilomita.

Kiplimo alienda mbele kidogo na Tenai.Lakini akawa anatazama nyuma mara kwa mara huku akikimbia.Komen alikimbilia nyuma kidogo na Tenai na alifanya kila kitu Tenai alifanya.

Kila wakati Tenai aliongeza mwendo naye Komen aliongeza. Baada ya muda mfupi, kila kijana alikuwa amebaki nyuma ya Komen, Tenai na Kiplimo.

Walipofika kati ya mwendo, hao watatu walikuwa mbele ya vijana wengine wote kiasi cha kilomita mbili.

Mwendo wa hawa watatu ulikuwa unafurahisha sana.Wawili wao walikuwa warefu kiasi na mmoja wao alikuwa mfupi wa kimo.Na wote walikuwa wanakimbia wakipanda na kushuka vilima.

Walipokuwa wamebakisha kilomita sita kumalizia mbio, Komen aliamua kukimbia kabisa.

Aliongeza mwendo na kumpita Tenai. Tenai alicheka alipoona huyo kijana mdogo akimpita. Alijua atampita watakapofikia kilima cha mwisho kabla ya kumaliza mbio.

Lakini Kiplimo hakutaka kupitwa na huyu kijana Komen.Wakati Komen aliongeza mwendo hata Kiplimo naye aliongeza mwendo.

Komen alikumbuka vile yule bibi wa Gari la Passat alimkimbiza.Alikumbuka pia bibi yule alivyoongeza mwendo wakati Komen alikuwa amechoka kabisa na anahema.

Komen alijua kwamba Kiplimo hataweza kustahimili huo mwendo wa kasi.

Kiplimo alipunguza mwendo wakati alitambua kwamba Komen hatapunguza.Komen alimpita na kuenda mbele yake.

Wakati huu Tenai alikuwa ametambua kwamba Komen hatapunguza mwendo.Kwa hivyo alikuwa ameongeza mwendo ili ampite.

Lakini Tenai aliona anakaribia sana Kiplimo; lakini mwendo kati yake na komen ulizidi kuongezeka.

Komen aliongeza mwendo alipoanza kupanda kilima cha mwisho kabla ya kufikia kimalizio.

Kwa wakati huu alikuwa kama mwendo wa kilomita moja na nusu mbele ya Tenai ambaye alikuwa amempita Kiplimo.

Alipofika juu ya kilima, Komen alikuwa anahisi kama kifua kinapasuka.Lakini alijua kwamba Tenai alikuwa amemfuata kwa kasi.

Komen alijaribu kuongeza mwendo wakati alifikia karibu na kikomo lakini hakuweza.Hii ni kwa sababu alikuwa amekembia kwa muda sasa kwa mwendo wa juu kupita kiasi chake kwa dakika kumi.

Mbele yake Komen aliwaona walimu wake na wafanyi kazi wa shule ambao walikuwa wakimtazama kwa mshangao.

“KOMEN, ULIWEZA kukimbia kwa muda wa dakika hamsini na tatu.Je utafanya vivyo hivyo tukikupa shilingi elfu hamsini?”

Alikuwa mwalimu mkuu akizungumza naye Komen baada ya wiki moja.Komen alikuwa anaenda kuwakilisha shule yake kwa riadha ya magwiji huko Nakuru wiki moja baadaye.

Mwalimu mkuu alitaka Komen awe bora kuliko wengine wote.Hili lingeongeza umaarufu wa shule yake.

Nitajaribu niwezavyo mwalimu.” Komen alijibu kwa heshima.Wakati huu komen alikuwa ameonja uzuri wa kuwa gwiji.

Kuanzia siku ile aliyoshinda hizo mbio hakuna mtu shuleni aliyesema kitu kwake.Hata mkuu wa wanafunzi katika shule hiyo alikuwa anamsifu.

Alitolewa kwa ratiba zote za kazi za shule.Hakuwa sasa anaosha bweni Jumamosi au darasa siku za shule.

Mbio za magwiji za Nakuru zilikuwa mteremko kwake komen.Aliwashinda washindani wake wote kwa muda wa dakika hamsini na tano.Aliyekuwa kwa nafasi ya pili alimaliza dakika kumi nyuma yake.

Kitu cha muhimu sana katika mbio hizo ni kwamba mkuu wa riadha Kenya Bwana Isaya Kiplagat alimwona.

Na Bwana Isaya alimwambia kwamba atashiriki Mashindano ya Magwiji ya “Half Marathon” ya Ulimwengu huko Boston Marekani.

Hili lilimshangaza Komen.Hakutarajia kushiriki mashindano yoyote ya kiwango cha dunia hivi karibuni.Alifikiri kuwa lazima angefikisha umri wa kisheria ili akubaliwe.

“Hakuna talanta ambayo haijakomaa. Tutashughulikia stakabadhi zote zinazohitajika katika safari.

Baba yako ndiye ataweka sahihi kwa stakabadhi zako.” Kiplagat alimwambia.

“Ni sawa. Nimeshukuru sana kwa kunipa hii fursa.”Komen alisema.

KOMEN alisafiri hadi Boston na wanariadha wengine wane. Wote walikuwa wanaenda kushindana kwa mbio za Half Marathon.Hao wote walikuwa wakubwa wake.

Mmoja wao alikuwa anaitwa Kiptanui, mwingine Kemei, wa tatu Kandie na wa nne Rono.Kusafiri kwa ndege kwa muda wa saa ishirini na nne lilikuwa ni jambo kuu kwake.

Mshindi wa Mbio za Nusu Marathon mwaka huo angezawadiwa dola elfu mia moja.Hiyo ni kama shilingi millioni nane za Kenya.

Siku ambayo walikuwa wanakimbia kulikuwa na joto jingi sana ukilinganisha na maeneo nchini Kenya.Komen alifuata maagizo aliyokuwa amepewa.

Alikunywa maji lita tatu saa moja kabla ya mbio kuanza.

Jambo zuri katika mbio hizo ni kwamba barabara waliyofuata ilitengenezwa vizuri.Haikuwa na kishimo hata kimoja.

Walioshiriki katika mbio hizi walikuwa watu mia tatu. Komen alijua kwamba wengi wao walikuwa wale wa kuthibiti mwendo.

Hakuwa na wasiwasi wakati walianza kukimbia kwa mwendo wa kasi sana.Baada ya kilomita moja, wakimbiaji mia moja walikuwa wamejiuzulu.

Wakati walifikia kilomita mbili, walisalia kama wakimbiaji mia moja.Hapo ndipo Komen aliongeza mwendo kidogo.

Walipomaliza kilomita kumi, Komen aliongeza mwendo tena na sasa alikuwa anakimbia kwa mwendo wa kasi kuliko vile alivyoanza.Kwa wakati huu alifikia nafasi ya kumi.

Mbele yake kulikuwa na Mkenya mwenzake Kandie.Kemei, Kiptanui na Rono walikuwa wakikimbia kama kikundi.Wote walikuwa nyuma yake.

Wazungu wengine wawili walijiuzulu na sasa Komen akakuwa nambari nane.Dakika chache baadaye, Kemei, Kandie na Rono wakamfikia.

“Jaribu kukimbilia karibu nasi. Hizi mbio ni za Wakenya,” Kemei alimwambia kwa Kiswahili.

Komen aliongeza mwendo kidogo ili awe karibu nao.Lakini baada ya kumaliza kilomita moja, alihisi ni wakati wake kuongeza mwendo tena.

Alijua anakimbia nao na tena hakimbii nao.Ilimlazimu atumie sheria zake yeye mwenyewe.

Aliongeza mwendo na kuwapita wakimbiaji wengine wote. Sasa akawa nambari ya kwanza.

Alipoona kwamba umebaki mwendo kama wa kilomita tatu hivi, aliamua kutimua mbio hadi amalize.

Wengine waliotamani kumpita wakafa moyo walipoona kuwa anaongeza mwendo.

Wanariadha hawakujaribu hata kumfuata walipogundua huo ndio mwendo wake mpaka mwisho wa mbio.

Alimaliza kilomita moja mbele ya washindani wenzake wote.

KILA MTU nchini Kenya akafurahia sana.Ulikuwa wakati wa kwanza mwanafunzi wa shule ya upili kushinda mbio za Dunia.Je kijana wa aina gani!

Ana umri wa miaka kumi na mitano lakini gwiji.Ndege yao ilipotua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, watu wengi sana walifika kumsubiri.

Kamera zilikuwa zimemwelekea hata kabla hajaanza kutoka kwa ndege.

Kati ya watu waliofika kumlaki ni wazazi wake, mwalimu mkuu wa Iten Bwana Arap Samoei na watu wengine wengi. Kila mtu alikuwa akicheza huku wakisifu jina lake.

Baada ya kunywa maziwa iliyochacha, aliongozwa na wazazi wake na askari wachache hadi kwenye gari la Passat.

Alishangaa kumwona yule bibi aliyemkimbiza akiwa katika shule ya msingi miaka miwili ilyopita.

“Wewe ni nani?” Komen aliuliza baada ya kuketi katika kiti cha kushoto upande wa nyuma ya gari.

“Umeshangaa Komen. Huyu ni shangazi yako Hilda Chepkemoi. Yeye naye ni Gwiji wa mbio za Marathon.” Babake alimwambia.

“Kumbe wewe ni shangazi yangu? Kwa nini hukuniambia?” Komen aliuliza huku gari lao likielekea kati kati ya jiji la Nairobi.